MAMBO 10 AMBAYO MWANAUME HUPENDA KUSIKIA TOKA KWA MPENZI WAKE.
10. Kukosolewa – “I think you are wrong” 👉Wanaume wanaweza kujikweza sana lakini daima hawachukii kurekebishwa. 👉Wanachojali zaidi ni jinsi gani au njia gani imetumika kuwarekebisha. 👉Mwanaume akikosea, anataka mpenzi wake amkosea lakini kwa mapenzi, sio kwa mikwaruzano au dharau au mbele ya kadamnasi. Mrekebishe au mkemee faragha, toa maoni yako na wala usimlazimishe, itamfanya aone unajali na unataka kumjenga. 9. Kujali – “How was your day?” 👉Wanawake wengi hutaka wao tu ndio waulizwe kuhusu jinsi siku zao zilivyoenda kila siku, wanasahau kabisa hata wanaume nao walikua kwenye mihangaiko. 👉 Mzoeshe kumuuliza mpenzi wako siku yake ilikuwaje? utaona hata nuru ya mapenzi yenu itang’aa na mtakua marafiki, japo mwanzoni atakua hakuambii kila kitu lakini baada ya muda atazoea. 👉 Kila mtu anataka wa kumsikiliza, mtu atakayezungumza nae chochote kilichotokea ndani ya siku yake, na pengine kukuuliza ushauri. 8. Ucha Mungu – “Can we pray?” 👉Mwanaume, anayesali au k...